Share this to

By:Hassan Pojo

Wakazi wa Jomvu wanatarajiwa kunufaika na elimu ya ufundi baada ya Serikali ya Kitaifa kutenga shilingi milioni 39 kwa ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha TVET katika eneo bunge hilo.

Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib, alitangaza hayo wakati wa mahafali ya wahitimu wa Chuo cha St. Mulumba Technical and Vocational College, Mikindani.

Badi alisema ujenzi wa chuo hicho, ambao umeidhinishwa na Rais Dkt. William Ruto, utapanua fursa za mafunzo ya ufundi kwa vijana wa Jomvu na maeneo ya jirani, kuwapa ujuzi wa kujiajiri na kuongeza nafasi za ajira.

Aliwapongeza wahitimu kwa juhudi zao na kuwataka kutumia maarifa waliyopata kuchangia maendeleo ya jamii na taifa.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu Dominic Kimengich aliwahimiza wahitimu kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na ubunifu wanapoingia katika soko la ajira.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *