Share this to

By:Hassan Pojo

Viongozi wa kisiasa kutoka ukanda wa Pwani wamekutana katika kikao cha mashauriano kujadili mikakati ya kuharakisha maendeleo ya eneo hilo, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Madini na Uchumi wa Buluu Ali Hassan Joho, Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, Mbunge wa Jomvu Badi Twalib pamoja na viongozi wengine kutoka kaunti za Pwani.

Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali za kaunti na serikali ya kitaifa ili kuongeza ajira kwa vijana, kuvutia uwekezaji, kuimarisha biashara, utalii, uchumi wa buluu na kuboresha miundombinu.

Pia walikubaliana kuwekeza zaidi katika elimu, mafunzo ya ufundi na uwezeshaji wa vijana kiuchumi, wakisema maendeleo ya Pwani yatafanikiwa kupitia umoja wa viongozi na mashauriano ya mara kwa mara yanayolenga maslahi ya wananchi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *