Share this to

By:Glory Mwagambo

Wakazi wa Malindi, Kaunti ya Kilifi, wamelalamikia uhaba wa maji unaodumu kwa muda mrefu, wakisema tatizo hilo limekuwa la kawaida licha ya ahadi zilizotolewa na serikali ya kaunti kulitatua.

Mmoja wa wakazi hao, Ali Juma, amesema idara ya maji imezembea katika kutekeleza wajibu wake, jambo ambalo limechangia kuendelea kwa tatizo hilo. Ameeleza kuwa, licha ya ahadi zilizotolewa na Gavana wa Kaunti ya Kilifi, wakazi bado hawajaona mabadiliko yoyote.

Kwa mujibu wake, wakazi hupata maji mara mbili pekee kwa mwezi, huku wakiendelea kulipa bili kubwa ambazo hawafahamu zinatokana na matumizi yapi. Aidha, amesema maji yanapotoka huwa ni nyakati za usiku pekee, hali inayowalazimu wengi kukesha ili kuyachota.

Mwambire amesema tatizo hilo limekuwa likijirudia kila mwaka, na kuwataka viongozi pamoja na idara husika kuchukua hatua za kudumu ili kuhakikisha wakazi wa Malindi wanapata huduma ya maji ya uhakika.

Wakazi hao wameiomba serikali ya kaunti na mamlaka zinazohusika kuharakisha utekelezaji wa suluhu za kudumu ili kukomesha changamoto hiyo ambayo imeendelea kuwaathiri kwa muda mrefu.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *