Share this to

By:Menza Ali

Kamati ya Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF) katika Eneo Bunge la Changamwe, Kaunti ya Mombasa, imeanza mchakato wa kubaini na kupanga utekelezaji wa miradi mipya ya maendeleo, baada ya kukamilika kwa miradi iliyopendekezwa awali na wananchi.

Akizungumza baada ya mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi, mjumbe wa hazina hiyo, Abdulhakim Ali, amesema miradi kadhaa tayari imekamilika, ikiwemo ujenzi wa taasisi za elimu pamoja na mipango ya kuhifadhi na kuboresha mazingira.

Abdulhakim amesema maoni ya wananchi yataendelea kuwa msingi muhimu katika kubuni miradi itakayolenga kushughulikia mahitaji halisi ya wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya NG-CDF ya Eneo Bunge la Changamwe, Halid Kabanda, amepongeza ushiriki wa wananchi katika kutoa mapendekezo ya miradi ya maendeleo, akisema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa miradi yenye manufaa kwa jamii.

Baadhi ya wananchi waliowasilisha mapendekezo yao wameitaka kamati hiyo kuzingatia kuwapa fursa wakandarasi wa eneo hilo katika utekelezaji wa miradi, ujenzi wa barabara za lami, uwekaji wa taa za mitaani pamoja na kuimarisha shughuli za utunzaji mazingira.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *