Kabla ya mradi huu kuja walimu shuleni pamoja na wanafunzi walikuwa wanalima kwa mbinu zao za kawaida za asili ikiwemo kuweka mbolea, lakini unakuta hata kuvuna walikuwa hawavuni kama inavyopaswa, ni kauli ya mnufaika wa mafunzo ya kilimo bora shuleni yaliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania. Emile Mfamwo, mwalimu na pia Afisa Elimu, Taalum wilaya ya Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ulioko kaskazini-magharibi mwa Tanzania alikuwa anazungumzia mafunzo hayo yaliyotolewa kwa walimu kwa ushirikiano kati ya FAO na shirika la Uchumi na Maendelo ya Jamii Vijijini (RECODA) chini ya utekelezaji wa Programu ya Pamoja ya Kigoma, KJP, awamu ya pili ndani ya Halmashauri ya Buhigwe

