Hivi karibuni hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Anold Kayanda alipata wasaa wa kuzungumza na Gloria Anderson Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI yaani Tanzania Enlightment and Development Innovation, Shirika lisilo la kiserikali kutoka Tanzania linalojishughulisha na miradi ya maendeleo ya elimu na vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo kwa kuwawezesha wananchi kiteknolojia katika zama hizi ni kuwapa nyenzo ya kujikwamua katika umaskini. Gloria anaanza kwa kueleza ushiriki wake katika Mkutano wa Zama Zijazo uliofanyika hapa hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.

