Share this to

By:Gloria Mwagambo

Wito umetolewa kwa Serikali ya Kaunti ya Kilifi pamoja na wadau wa michezo na wahisani kujitokeza kusaidia kikundi cha vijana cha KD United kinachoshiriki mchezo wa mpira wa wavu mjini Malindi ili kiendelee kukuza vipaji na kuwaepusha vijana na mienendo hatarishi.

Kocha wa timu hiyo, Andrew Nzulu, amesema KD United imekuwa jukwaa muhimu la kuwaokoa vijana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, uhalifu na mimba za mapema kupitia ushiriki wao katika michezo.

Hata hivyo, Nzulu amesema timu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha, hali inayowalazimu wakati mwingine kukosa kushiriki mashindano mbalimbali. Ameitaka Serikali ya Kaunti ya Kilifi pamoja na wadau wengine wa michezo kuingilia kati kwa kutoa ufadhili ili kuhakikisha mchezo wa mpira wa wavu unaendelea kukua na vipaji vya vijana vinanolewa.

Kauli hiyo imeungwa mkono na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Regina Kinyili, ambaye amewahimiza vijana wenza wake kujiunga na KD United ili kujiepusha na matumizi ya mihadarati, uhalifu na mimba za mapema. Aidha, ametoa wito kwa wahisani na wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia timu hiyo kifedha ili iweze kushiriki mashindano na kuendelea kukuza vipaji vya vijana.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *