Share this to

By:Robert Mutasi

Utafiti mpya wa taasisi ya TIFA umeonyesha mabadiliko makubwa katika siasa za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, huku Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna akiibuka kama mwanasiasa anayepata uungwaji mkono kwa kasi zaidi.

Kulingana na matokeo ya utafiti huo, umaarufu wa Sifuna umeongezeka kutoka asilimia sifuri mwaka jana hadi asilimia 15 mwezi Juni mwaka huu, na kumfanya kuwa kiongozi wa upinzani aliyepata ongezeko kubwa zaidi.

Wakati huo huo, viongozi wengine wa upinzani wameonyesha kushuka kwa umaarufu, ambapo Kalonzo Musyoka ameshuka kutoka asilimia 25 hadi 13, Fred Matiang’i kutoka asilimia 32 hadi 14, huku Rigathi Gachagua akipata asilimia 7.

Kwa upande wa serikali, Rais William Ruto anaendelea kuongoza kwa asilimia 24 ya uungwaji mkono.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 20 ya Wakenya bado hawajafanya uamuzi kuhusu mgombea watakayemuunga mkono katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Ndani ya vyama vya kisiasa, Edwin Sifuna anaongoza kwa uungwaji mkono ndani ya ODM kwa asilimia 44, huku Rais William Ruto akiongoza ndani ya UDA kwa asilimia 84.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *