Share this to

By:Hassan Pojjo

Makundi ya mashindano ya mpira wa wavu ya Kenya Primary and Junior Schools Sports Association (KPJSSA) Kanda ya Pwani mwaka 2026 yametangazwa, huku timu kutoka kaunti sita zikijiandaa kuwania tiketi ya mashindano ya kitaifa.

Mashindano hayo yatafanyika tarehe 26 na 27 Julai 2026 katika viwanja vya Kwale High School, yakiwakutanisha mabingwa wa shule za msingi na Junior Secondary School (JSS) kutoka Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Taita Taveta na Lamu.

Kwa upande wa wasichana wa shule za msingi, Kundi A linaundwa na Kwale, Mombasa na Tana River, huku Kundi B likiwa na Kilifi, Taita Taveta na Lamu.

Kwa wavulana wa shule za msingi, Kundi A lina Kwale, Tana River na Taita Taveta, wakati Kundi B linajumuisha Kilifi, Lamu na Mombasa.

Katika ngazi ya Junior Secondary School (JSS) kwa wasichana, Kundi A lina Kilifi (St. Andrews), Taita Taveta na Kwale, huku Kundi B likiwa na Mombasa, Lamu na Tana River.

Kwa upande wa wavulana wa JSS, Kundi A linaundwa na Kilifi (St. Andrews), Mombasa na Lamu, wakati Kundi B lina Kwale, Tana River na Taita Taveta.

Mashindano hayo yanatarajiwa kushuhudia ushindani mkali huku yakitumika kuchagua timu zitakazoiwakilisha Kanda ya Pwani katika mashindano ya kitaifa ya KPJSSA.

Waandalizi wamesema maandalizi yote yamekamilika na timu zinatarajiwa kuwasili Kwale kabla ya kuanza kwa mashindano, huku walimu, wazazi na wadau wa michezo wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kuwapa hamasa wanafunzi watakaoshiriki.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *