By:Hassan Pojjo

Zaidi ya wanawake 500 kutoka vikundi 24 vya wajane katika Wadi ya Dzombo, Kaunti ya Kwale, wamenufaika na mpango wa uwezeshaji wa kiuchumi unaoendeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa, Dkt. Raymond Omollo.
Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa msaada huo, Dkt. Omollo alisema serikali itaendelea kuunga mkono programu za kuwawezesha wajane, wanawake na vijana ili kuboresha maisha yao na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Viongozi waliohudhuria, akiwemo Seneta wa Kwale Raphael Chimera, waliipongeza programu hiyo wakisema itawasaidia walionufaika kuanzisha na kupanua biashara ndogo ndogo. Wanawake walionufaika walishukuru kwa msaada huo wakisema utawainua kiuchumi na kuboresha maisha ya familia zao.
