By:Farida Ali

Wito wa nafasi ya naibu rais waongezeka Magharibi mwa Kenya huku washirika wa Spika Moses Wetang’ula wakimshinikiza Rais William Ruto kuzingatia eneo hilo katika uchaguzi wa mwaka 2027.
Viongozi hao wanasema matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge Ol Kalou ni ishara kuwa uungwaji mkono wa serikali ya Kenya Kwanza katika eneo la Mlima Kenya haupaswi kuchukuliwa kuwa wa moja kwa moja.
