Share this to

By:Farida Ali

Spika wa Bunge Moses Wetang’ula amewataka viongozi wa makanisa Magharibi mwa Kenya kuongoza kampeni ya kuwahamasisha wananchi kujisajili kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Wetang’ula amesema mamia ya maelfu ya watu wenye vitambulisho vya kitaifa katika kaunti za Kakamega na Bungoma bado hawajajisajili na IEBC.

Spika huyo pia ametetea miradi ya serikali ya Rais William Ruto Magharibi mwa Kenya, akisema imechangia ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.


Share this to

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *