
Vijana wa Coast United Football wasiozidi miaka 17 kutoka wodi ya Magogoni eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa wanaoshiriki michuano ya FKF ya mkufunzi Mohammed Mng’aro na Rama Changawa wanarindima kwenye gemu hizo.
Gemu ya Coast United Football dhidi ya Mablanda walinyukwa bao 1-0 ugenini, huku vijana hao wakiendelea kupata kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Mombasa kings.
Coast United walipata kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya vijana wa Rival, aidha Coast United walipata wanyonge wao Babito na kuwafunga mabao 2-0.
Timu ya PNI iliwaburuza Coast United mabao 2-0 huku vijana wa Valley nao wakiwa hapa mabao 2-0.
Kulingana na mkufunzi wa Coast United Football Mohammed Mung’aro ni kwamba jumamosi watakuwa na gemu na timu ya volcano eneo la jomvu.
